Tuzo za Muziki za Tanzania zinazodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Lage (KTMA2014), zilifanyika jana Mei 3 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo Diamond Platinumz aliibuka kuwa mshindi wa tuzo saba.

Diamond alishinda tuzo ya Muimbaji bora wa kiume-Kizazi kipya,Video bora ya mwaka (My Number One), mtumbuizaji bora wa kiume –Kizazi kipya, Mtunzi bora wa mwaka – Kizazi Kipya, Wimbo bora wa Afro Pop, Wimbo bora wa mwaka na Wimbo bora wa kushirikiana alioshirikishwa na Nay wa Mitego (Muziki Gani).

 Angalia picha mbalimbali za washindi wa tuzo za #KTMA2014 na wasanii waliotumbuiza pamoja na watu waliohudhuria wakiwepo mastaa.








 





 Angalia orodha kamili ya washindi KTMA2014:


Wimbo bora wa mwaka
Number One – Diamond 

Mwimbaji bora wa kike – kizazi kipya
Lady Jaydee

Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya
Diamond

Muimbaji bora wa kike taarab
Isha Ramadhan

Muimbaji Bora wa kiume – Taarab
Mzee Yusuf

Muimbaji bora wa kiume – Bendi
Jose Mara

Muimbaji Bora wa Kike – bendi
Luiza Mbutu

Msanii Bora wa Hip Hop
Fid Q

Msanii Bora Chipukizi Anayechipukia
Young Killer

Rapa Bora wa Mwaka – Bendi
Furguson

Mtumbuizaji bora wa kike muziki
Isha Ramadhani

Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki
Diamond

Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop
Fid Q

Video Bora ya Mwaka
Number One – Diamond

Bendi ya Mwaka
Mashujaa Band

Kikundi cha Mwaka cha Taarab
Jahazi Modern Taarab

Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya
Weusi

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Taarab
Enrico

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Kizazi kipya
Man Walter

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Bendi
Amoroso

Mtunzi Bora wa Mwaka – Taarab
Mzee Yusuf

Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya
Diamond

Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi
Christian Bella

Wimbo bora wa Kiswahili – Bendi
Ushamba Mzigo – Mashujaa Band

Wimbo bora wa reggae
Niwe na Wewe – Dabo

Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Tubonge – Jose Chameleone

Wimbo bora wa Afro Pop
Number One – Diamond

Wimbo bora wa Taarab
Wasiwasi Wako – Mzee Yusuf

Wimbo bora wa Hip Hop
Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako

Wimbo Bora wa R&B
Closer – Vanessa Mdee

Wimbo Bora wa Kushirikiana
Muziki Gani – Nay wa Mitego ft Diamond

Wimbo bora wa ragga/dancehall
Nishai – Chibwa f/ Juru

Wimbo bora wa zouk /rhumba
Yahaya – Lady Jaydee

Hall of FAME Award
Hassan Rehani Bichuka
Masoud Masoud & TBC Taifa 











 
Top