TIMU yaTaifa ya Italia maarufu kama Azzuri imeangukia pua usiku huu katika mchezo wa kombe la dunia kundi D baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Costa Rica.
Costa Rica wamepata ushindi wa pili katika kundi lao kwani mchezo w aufunguzi waliwafunga Uruguay mabao 3-1.
Kwa matokoe hayo, Costa Rica wamefuzu kwa mara ya kwanza hatua ya 16 tangu mwaka 1958.
Bao pekee la Costa Rica limefungwa na Bryan Ruiz katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.
Bryan Ruiz akishangilia bao lake katika kipindi cha kwanza.