Muangalizi: Jose Mourinho (kulia) amekuwa akiwatembelea watoto wanaosumbuliwa na njaa pamoja na wagongwa wa UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama balozi wa Mpango wa Chakula Duniani.
BOSI wa Chelsea, Jose Mourinho anadhani chama cha soka nchini England, FA kingetoa faini za mpira wa miguu anazolipa kwa kuwasaida watu wenye shida kama sehemu ya upendo.
Badala ya kuangalia kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil, Mourinho amewatembelea watoto wanaosumbuliwa na njaa na wagonjwa wenye virusi vya UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama balozi wa umoja wa mataifa wa Mpango wa Chakula Dunia.
Mreno huyo alisema anataka kuona mpira unafanya kazi zaidi kusaidia mpango wa Chakula Duniani (WFP) na akapendekeza FA itumie faini anazotozwa kuwasaidia watu wenye shida.
“Nitalipa (faini) kwa tabasamu kama hela zinakwenda sehemu sahihi,” Aliwaambia ITV wakati wa ziara yake.
‘Huo ni uzoefu, kwakweli nimepata uzoefu,”. Alisema kocha huyo mwenye miaka 51 huku akishindwa kuzuia machozi yaliyokuwa yanamlenga.
“Na aina ya uzoefu ambapo najisikia kidogo”.
“Ni machungu, lakini wakati fulani huwa ni nzuri kwa roho”.
Mpango wa Chakula Dunia ni shirika kubwa la kimataifa linaloshughulikia balaa la njaa duniani kote.
Mwezi mei, Mourinho alitozwa faini na FA ya Euro 10,000 kwa maneno yake aliyosema juu ya viongozi wa mechi baada ya Chelsea kufungwa mabao 2-1 na Sunderland na kujikuta akivunja rekodi ya kucheza mechi 77 bila kufungwa nyumbani.
Mourinho baada ya kutembelea Afrika amesisitiza faini zinazotozwa ligi kuu zipelekwa kusaidia wenye shida.