Malinzi
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
RAIS wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi, jana aliwaalika waandishi wa habari akiwaomba wafike leo mchana majira ya saa 6:00 katika ofisi za shirikisho hilo kwa lengo la kutoa ujumbe kwa umma wa wapenda michezo Tanzania.
Wengi hawakupata majibu juu ya nini Rais Malinzi anataka kuzungumza na wanahabari kwasababu si kawaida yake kufanya mikutano na waandishi mara kwa mara.
Akitokea Brazil kwenye mkutano wa 64 wa FIFA hivi karibuni, hatimaye mchana wa leo, Rais Malinzi amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo, uliopo makao makuu katikakati ya jiji la Dar es salaam na kutangaza kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba ulioatarajia kufanyika juni 29 mwaka huu hadi hapo itakapounda kamati ya Maadili itakayokuwa na jukumu la kusikiliza masuala ya maadili kuelekeza uchaguzi huo.
Rais Malinzi amesema Simba inatakiwa kukamilisha zoezi hilo la kuunda kamati ya Maadili hadi kufikia juni 30 mwaka huu ili mchakato wa uchaguzi uweze kuendelea chini ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, wakili, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro.
Wengi walijiuliza kwanini TFF imefikia uamuzi huo, lakini Malinzi alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia kuibuka kwa malalamiko mengi ya kimaadili, hivyo kamati hiyo itayasikiliza na kufikia maamuzi.
Uchaguzi wa Simba uliopangwa kufanyika juni 29 mwaka huu uliingia sura mpya tangu Michael Richard Wambura aliopoenguliwa kugombea nafasi ya Urais.
Suala hilo lilionekana kugusa watu wengi, lakini alipokata rufani na kushinda, mengi yakaibuka zaidi na baadhi ya wanachama walipinga kurudishwa kwake katika uchaguzi wa Simba.
Hata hivyo, Malinzi amekiri kuwa TFF imepokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo, hivyo ni muhimu kuundwa kwa kamati ya maadili itakayoshughulikia mambo hayo.
rage 2Ismail Aden Rage na kamati yake ya Utendaji wataendelea kuiongoza klabu ya Simba sc.
Wakati huu ambapo kamati itakuwa ikiundwa, kamati ya utendaji ya Simba iliyopo madarakani kwasasa, chini ya Rais wake, Ismail Aden Rage itaendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Jana Rage wakati anazungumza na mtandao huu alisema anajitahidi kuhakikisha anaacha mchoro au msingi au hata ghorofa moja ya Hosteti za wachezaji katika eneo lake la Bunju ili kuepukana na gharama kubwa wanazotumia kuwaweka wachezaji hotelini wanapofanya kambi.
Rage aliyasema hayo kufuatia uongozi wake kuanza utekelezaji wa ujenzi wa uwanja wa kisasa ambapo tayari magereda na malori yalishapelekwa kwajili ya kazi.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2137#sthash.ag5vTiqv.dpuf
 
Top