maximo
Kocha Mkuu mpya wa Yanga Marcio Maximo (kushoto)akiwa na Afisa Habari Baraka Kizuguto, Katibu Mkuu Beno Njovu na kocha msaidizi Leonadro Neiva mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere
Kocha Mbrazil Marcio Marcel Maximo tayari ameshawasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuanza kazi kukinoa kikosi cha timu ya Young Africans kwa ajili ya msimu ujao kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kimataifa.
Kocha Maximo ambaye awali aliwahi kufanya kazi nchini akiwa kama Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) amewasili mchana wa leo akiwa na msaidizi wake Leonadro Martins Neiva kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini na kulakiwa na umati mkubwa uliokuwa umejitokeza kumlaki.
Mara baada ya kuwasili kocha Maximo pamoja na msaidizi wake Neiva walipokelewa na Katibu Mkuu wa Yanga SC Bw. Beno Njovu ambapo mara baada ya kukamilisha masuala yote ya uhamiaji walitoka nje na kuwapungia mikono washabiki, wapenzi na wanachama waliokuwepo uwanjani hapo
Kuhus ujio wake Tanzania kujiunga na klabu ya Yanga SC Maximo alisema kesho ataongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani majira ya saa 5 kamili asubuhi ambapo ndipo atapata fursa ya kueleza kila kitu juu ya ujio wake.
Aidha kesho majra ya saa 8 kamili mchana kiungo mshambuliaji Andrey Macrcel Ferreira Coutinho anatarajiwa kuwasili kwa shirika la Ndege la Afrka Kusini tayari kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Young Africans kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2014/2015.
Wapenzi, wanachama, na washabiki wa Young Africans mnaombwa kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Ndege wa JK Nyerer kumpokea kiungo huyo ambaye amesema anakuja kufanya kazi nzuri nchini na kuisaidia Yanga kwenye michuano mbalimbali. 
Chanzo: Tovuti ya Yanga

 
Top