????????
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba sc, Zacharia Hans Poppe
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MWENYEKITI wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe ataendeleza kuiongoza kamati hiyo katika uongozi mpya ulioingia madarakani juni 29 mwaka huu.
Rais mpya wa Simba sc, Evans Elieza Aveva ametangaza kumteua Poppe kuendelea kuwa mwenyekiti, huku Kassim Mohammed Dewji akiteuliwa kuwa makamu mwenyekiti.
Aveva pia amewateua wajumbe wa kamati hiyo ya usajili ambao ni Said Tuliy, Musley Al Ruwaih, Crescentius Magori na Dk Roadney Chiduo.
Rais Aveva pia ameunda kamati mbili, moja ya soka la vijana na kamati ya mashindano.
Kamati ya soka la vijana itakuwa chini ya mwenyekiti wake Said Tully. Wajumbe wengine ni Ally Suru, Patrick Rweyemamu, Mulamu Nghambi, Madaraka Suleiman na Amina Poyo.
Kamati ya Mashindano itaongozwa na mwenyekiti Mohammed Nassor, huku Makamu mwenyekiti akiwa ni Iddi Kajuna na Wajumbe wengine ni Jerry Yambi, Hussein Simba na Mohammed Omar.  
     Kwa mamlaka aliyonayo kikatiba, Aveva amewateua  Mohammed Nassor, Musleh Al Ruwaih na Salim Abdallah kuwa wajumbe wa  Kamati ya Utendaji.
Katika hatua nyingine kikao kilichokaa jana kwa mara ya kwanza tangu Aveva aingie Madarakani kiliamuakuwasimamisha uanachama, wanachama  69  waliokwenda  Mahakamani kuweka zuizi la uchaguzi kufanyika.
Aveva alieza kuwa maamuzi hayo yamefanyika ili kuilinda katiba ya Simba inayokataza masuala ya klabu kupelekwa katika mahakama za kawaida.
Suala kama hilo liliwahi kufanywa na Michael Richard Wambura mwaka 2010 na lilimgharimu katika uchaguzi wa mwaka huu.
Hata hivyo katika uchaguzi wa juni 29, Wambura alizuiliwa kupiga kura kwa madai ya uanachama wake kuwa na utata.
Lakini suala la Wambura na wanachama wengine kusimamishwa litaamuliwa katika mkutano mkuu wa wanachama unaotarajia kufanyika agosti 3 mwaka huuu.

 
Top