Germany-vs-Argentina-2014-World-Cup-Final-In-Brazil-Wallpaper-3840x2400
Na Baraka Mbolembole
 Michuano ya kombe la dunia nchini Brazil inatarajia kufikia tamati, Jumapili hii kwa mchezo wa fainali kati ya miamba miwili ya Amerika Kusini na Ulaya.
Argentina itapambana na Ujerumani katika uwanja wa Maracana, jijini, Rio De Janeiro. Mechi ya mshindi wa tatu itachezwa Jumamosi hii kwa wenyeji wa michuano, Brazil kupambana na Uholanzi.
Makocha, Luiz Filipe Scolari wa Selecao, na Luis Van Gaal wa Orange kwa pamoja wametoa ushauri kwa mchezo huo kufutwa katika fainali zijazo kwa maana hauna maana yoyote kwa ‘ washindwa hao wa michezo ya nusu fainali’.
article-2685267-1F7DC01800000578-918_634x637
Katika michuano hii ya 20 jumla ya zawadi ambazo hutolewa kwa timu shiriki 32 ni kiasi cha dola za Kimarekani, millioni 576. Vilabu vya Brazil vimepata kiasi cha dola millioni 70. Asilimia 37 ya kiwango cha pesa katika zawadi kimeongezeka kutoka katika michuano ya mwaka 2012 nchini Afrika Kusini. Kabla ya michuano kuanza kila timu ilipewa kiasi cha dola millioni 1.5 kwa ajili ya maandalizi.
 Fifa imegawanya zawadi hizo katika mafungu saba tofauti huku bingwa wa michuano akipata kiasi cha juu zaidi. Dola millioni nane zilitoka kwa timu 16 ambazo ziliondoshwa katika michuanohatua ya awali.
Timu ambazo zilipata mgawo huo ni kama Cameroon, Ivory Coast, GHana, Iran, Korea Kusini,Australia, Japan,Croatia, Bosnia, England, Italia, Hispania, na nyingine zilizoishia hatua ya awali hivyo ukitoa matokeo mabaya kwa timu hizo zilipata pesa ya kutosha.
 Kundi la pili la zawadi ni lile ambalo linahisha timu 16 ambazo zilifuzu kwa hatua ya 16 bora. Kiasi cha dola millioni tisa kilitolewa kwa kila timu ambayo ilishindwa katika mchezo wa hatua hiyo na kuondolewa mashindanoni.
Mexico, Chile, Uruguay, Algeria,Nigeria, Uswizi, Marekani na Ugiriki ndizo zilipata kitita hicho. Dola millioni 14 zilitolewa kwa timu nne ambazo zilishindwa katika michezo ya robo fainali.
Ufaransa, Colombia,Costa Rica na Ubelgiji ndiyo zilinufaika na malipo hayo. Timu ambazo zilishindwa katika nusu fainali zitapambana ili kupata washindi wa tatu na yule wa nne.
Timu itakayofungwa katika mchezowa kutafuta mshindi wa tatu katika ya Brazilna Uholanzi itapata kiasi cha dola millioni 20. Mshindi wa tatu atapata kiasi cha dola millioni 22.
Mshindwa katika mchezo wa fainali atapata kiasi cha dola millioni 25, na bingwa ataondoka na kiasi cha juu zaidi., dola za KImarekani millioni 35.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=3374#sthash.i8ctmCwe.dpuf
 
Top