Mwisho wa maisha Chelsea: Frank Lampard anajiunga na New York City FC.
Frank Lampard anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mchezaji mpya wa New York City FC leo majira ya saa 9.30 alasiri.
Mkutano na waandishi wa habari umetangazwa mjini New York kwa ajili ya kutambulisha mchezaji mpya na anatarajiwa kuwa nyota wa zamani wa Chelsea.
Tukio hilo litafanyika Brooklyn Bridge Park, ambalo pia litamhusisha Lampard kufundisha vijana 40 wa kliniki ya watoto ya Marekani.
Lampard alimaliza mkataba wake na Chelsea mapema majira haya ya kiangazi na hajaongezewa kandarasi nyingine.