11

BAADA ya kuenea kwa taarifa jioni ya leo kuwa Yanga sc imejitoa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kama Kombe la Kagame, uongozi wa Yanga umekanusha taarifa hizo.

Ilielezwa kuwa Yanga wameamua kujitoa katika michuano hiyo inayoanza kushika kasi Agosti 8 mwaka huu Mjini Kigali nchini Rwanda kwasababu kikosi chao hakijapata barua rasmi ya mwaliko.

Lakini ilisemekana kocha mkuu wa Yanga, Mbrazil , Marcio Maximo ameamua kujitoa kombe la Kagame kwasababu kikosi chake hakipo tayari kushiriki michuano yoyote ndani ya wiki mbili zijazo.

Kutokana na nusu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kuwepo katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania iliyoanza jioni ya leo mjini Tukuyu mkoani Mbeya, kocha Maximo ameona bora kujitoa.

Hata hivyo baada ya taarifa hizo, Yanga kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa facebook imesema kwamba haijajitoa kushiriki mashindano ya Kombe la Kagame chini Rwanda kama inavyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya habari nchini na kusema taarifa hizo ni za uongo.

 Katibu mkuu wa Yanga SC Bw Beno Njovu amesema taarifa hizo zilizosambazwa ni za uongo na kuwa kwa siku ya leo hajaongea na mwandishi wa habari yoyote juu ya michuano hiyo.

 “Sie hatujatangaza kutoshiriki michuano ya Kagame, kama tulivyosema awali kikubwa tunasubiri taarifa rasmi za kushiriki kutoka CECAFA


 
Top