Mchezo wa fainali za kombe la dunia mwaka 2014 kati ya Ujerumani na Argentina utapigwa majira ya saa nne usiku wa Jumapili katika uwanja wa Estadio Jornalista Mario Filho, maarufu kama Maraccana.
Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 78, 854 ni uwanja wa pili kwa ukubwa barani Amerika Kusini. Uwanja wa Maraccana ulitengenezwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya fainali za kombe la dunia mwaka 1950.
Unamilikiwa na Jimbo la Rio de Janeiro. Maraccana ni neno ambalo linatokana na kabila la Tupi-Guarani ambalo maana yake ni ndege aina ya Kasuku. Katika mchezo wa fainali za mwaka 1950 kati ya waliokuwa wenyeji Brazil na Uruguay uliweka rekodi ya kuingiza watazamaji wengi zaidi kwa wakati mmoja.
Mchezo huoambao ulimalizika kwa Uruguay kutwaa ubingwa kwa mabao 2-1 ulishuhudiwa na watazamaji wapatao 200, 000 ,idadi ya juu zaidi ya mashabiki katika historia ya soka.
Uwanja huo ni kama alama ya soka la Brazil na ni moja ya vivutio vikubwa vya Utalii nchini humo. Julai 19,1992 mashabiki watatu walikufa katika uwanja huo kutokana na kuanguka kwa moja ya majukwaa ya uwanja huo. Uwanja wa Maraccana umefanyiwa matengenezo mara kadhaa una thamani ya dola millioni 500.
Uwanja huo una migahawa,baa na maduka.Unaparking ya magari 14, 000 ambayo yanaweza kuingia katika uwanja huouliopo karibu na mto Rio Maraccana.
Argentina ilikuwa timu ya kwanza kuutumia uwanja huo katika michuano ya mwaka huu wakati wa mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya Bosnia Herzegovina.