download
Miroslav Klose amekuwa mfalme wa mabao katika fainali za kombe la dunia
Na Shaffid Dauda, Brazil ILIWACHUKUA nusu saa tu Ujerumani kufunga mabao 5-0 dhidi ya Brazil na hii imeweka historia katika njia nyingi. Hapa tunatazama ukweli kutoka nusu fainali ya jana usiku ambayo wenyeji walifungwa mabao 7-1.
UJERUMANI IMEPAA JUU ZAIDI
• Kwa kufunga bao la pili, Miroslav Klose amekuwa mfalme wa kufunga mabao katika fainali za kombe la dunia. Klose kwasasa amefikisha mabao 16 katika maisha yake ya soka na kuvunja rekodi ya Gwiji wa Brazil, Ronaldo.
• Ujerumani walifunga mabao 5 katika dakika 29 za kwanza, nchi hii imekuwa ya kwanza kufunga kwa haraka mabao matano katika muda wa mechi. Rekodi ilikuwa inashikiliwa na Yugoslavia ambao walifunga mabao matano katika dakika 30 dhidi ya Zaire mwaka 1974.
• Magoli 7 ya Ujerumani yamevunja rekodi ya mabao mengi zaidi kufungwa katika fainali za kombe la dunia, mwanzoni ilikuwa sita kati ya Uruguay na Argentina mwaka 1930, na Ujerumani Magharibi mwaka 1994. Hakuna aliyewahi kufunga hata mabao matano katika hatua ya nusu fainali tangu Brazil waifunge Ufaransa mabao 5-2 mwaka 1958.
Running riot: Germany scored four goals in six first-half minutes during Tuesday's semi-final against Brazil
• Bao la sita lilivunja rekodi ya mabao matano ya nusu fainali ya kombe la dunia. • Ujerumani sasa imekuwa nchi iliyofunga mabao mengi kwa wakati wote wa historia ya kombe la dunia. Imefunga magoli 223. Waliipita Brazil yenye mabao 220 katika kipindi cha kwanza kwenye mechi ya jana.
• Ujerumani wameweza kuongoza mara tatu kwa mabao matano  katika fainali za kombe la dunia- walifanya hivyo dhidi ya Saudi Arabia (2002) ambapo walishinda 8-0, walifanya hivyo dhidi ya Mexico mwaka 1978 waliposhinda mabao 6-0 na walifanya hivyo dhidi ya Uswisi mwaka 1966 waliposhinda 5-0.
•Ujerumani imefika fainali za kombe la dunia mara nyingi zaidi kuliko taifa lolote. Imefika fainali mara nane mpaka sasa.
  •  Thomas Muller anakuwa mchezaji wa 13 kufunga mabao 10 katika fainali za kombe la dunia na anakuwa mchezaji wa pili kufunga magoli matano mfululizo katika fainali za kombe la dunia baada ya Klose mwaka 2002 na 2006.
Disbelief: Fernandinho, Maicon and David Luiz look bemused following Germany's fifth goal of the evening
IMEISHUSHA HADHI BRAZIl
• Kipigo cha Brazil kimevunja rekodi yao waliyoweka mwaka 1920 walipofungwa mabao 6-0 dhidi ya Uruguay katika mchezo ya Copa Amerika.
• Brazil hawajawahi kufungwa mabao matano katika fainali za kombe la dunia tangu mwaka 1998. Waliruhusu mabao manne katika mechi tano mwaka 2010, mabao mawili katika mechi tano mwaka 2006 na mabao manne katika mechi saba za mwaka 2002.
• Brazil  haijawahi kufungwa mabao manne katika mechi yoyote ya kombe la dunia. Katika mechi zake 102 ilizocheza kabla ya jana.
• Brazil wameruhusu mabao matano mara nane kwenye michezo maalumu—sita mwaka 1960 au kabla na mara mbili mwaka 1963. Magoli sita? Sio,  tangu mwaka 1940. Saba? Sio,  tangu walipofungwa mabao 8-4 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Yugoslavia mwaka 1934.
• Rekodi mbaya ya nchi mwenyeji kufungwa mabao mengi ilikuwa mwaka 2010 ambapo Afrika kusini ilipoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Urugauy. Mexico ilifungwa mabao 4-1 na Italia mwaka 1970 na Sweden ilifungwa mabao 5-2 na Brazil mwaka 1958.
• Brazil imepoteza kwa mara ya kwanza  mechi za mashindano ilizocheza nyumbani tangu mwaka 1975 walipofungwa na Peru kwenye michuano ya Copa Amerika—imepita miaka 63.
• Kwa mara ya mwisho Brazil kupoteza mechi ya kombe la dunia nyumbani ilikuwa mwaka 1950 na kusababisha timu kubadili jezi zake
 
Top