Didier Drogba amekamilisha ndoto za kurejea Chelsea.
Nyota huyo wa Ivory Coast amesaini mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge.
Gwiji huyu alisainiwa kwa mara ya kwanza klabuni hapo na Jose Mourinho kwa dau la paundi milioni 24 mwaka 2004.
Drogba amefichua siri kuwa hakutaka kupoteza nafasi ya kufanya kazi tena na kocha Mourinho kwa mara nyingine tena.
Mshambuliaji huyu wa Ivory Coast amekamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Chelsea.
Alisema: “Yalikuwa maamuzi rahisi-nisingeweza kupoteza nafasi ya kufanya kazi tena na Jose. Kila mtu anajua mahusiano mazuri niliyokuwa nayo na klabu hii, na mara zote nimekuwa nikijisikia kama nyumbani”.
“Hamu yangu bado ni ileile na naangalia mbele kuisaidia timu hii. Namefurahia sana ukurasa huu mwingine wa maisha yangu ya soka”.
Mourinho amewaondoa hofu mashabiki wa klabu hiyo akisisitiza kuwa Muivorycost huyo bado ni mshambuliaji bora katika ulimwengu wa soka.
“Amekuja kwasababu ni miongoni mwa washambuliaji bora Ulaya. Namjua sana na najua kuja kwake hajivunia historia yake au kile alichofanya klabuni miaka ya nyuma”, Alisema Mourinho.
Mchezo wa mwisho kwa Drogba akiwa Chelsea ulikuwa wa UEFA ambao alifunga penati ya ushindi na kutwaa kombe hilo dhidi ya Bayern mwaka 2012.