Nyota wa mkopo: Lukaku alifanya vizuri alipokuwa Goodison Park mwaka jana na sasa Martinez anahitaji huduma yake tena.
EVERTON wanakaribia kumrudisha tena Romelu Lukaku katika dimba lao la Goodison Park.
Mbelgiji huyo ni mshambuliaji chaguo la kwanza la kocha Roberto Martinez majira haya ya kiangazi na anatarajia kukamilisha usajili wake ndani ya saa 48 zijazo.
Martinez, aliyekuwa anamfikiria demba Ba kama mbadala wa Lukaku, hakukubaliana na mshahara aliodai wa paundi elfu 80 kwa wiki, na sasa anataka kumshawishi mbelgiji mwenye miaka 21 kumwaga wino katika kikosi chake cha msimu ujao.
Inafahamika kuwa maandalizi makubwa ya kumrudisha Everton yamekamilika baada ya kurejea kutoka Austria walipoweka kambi.
Lukaku alikuwa anatarajia kusaini Atletico Madrid, lakini kwa bahati mbaya ikawa tofauti kwasababu hakuwa chaguo la kwanza la kocha Diego Simeone.
Wolfsburg pia walionesha nia kubwa ya kumsajili kama ilivyokuwa kwa Tottenham, lakini Lukaku alifurahia maisha Goodison na anapenda kuendelea kuisaidia klabu hiyo mpaka kufuzu ligi ya mabingwa.
Martinez pia amefanya mazungumzo ya kumrudisha mchezaji aliyekuwa kwa mkopo, Monaco, Lacina Traore.
Pia yupo katika makubaliano ya kumsajili kiungo wa Bosnia ,Muhamed Besic, mwenye miaka 21, anayekipiga klabu ya Ferencvaros.
-