Mtoto: Mourinho amesema hakutaka kumsajili Shaw kwasababu mshahara wake ni mkubwa sana.
JOSE Mourinho amesema hakuthubutu kutaka kumsajili Luke Shaw kwasababu mshahara aliohitaji kinda huyo `ungeua umoja’ wa timu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Shaw mwenye miaka 19, alisaini Manchester United kwa dau la paundi milioni 30 na inasemekana atakuwa analipwa mshahara wa paundi laki moja na elfu 20.
Mourinho alisema kiwango hicho ni kikubwa sana kwa klabu yake.
‘Kama unamlipa mshahara mkubwa kijana mwenye miaka 19 Luke Shaw, tulikuwa tunahitaji nini?, tungekufa’ alisema kocha wa Chelsea. “Tungeua umoja na utulivu wetu katika matumizi ya hela. Tungeua umoja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo”.
“Kwasababu unapomlipa zaidi mtoto wa miaka 19-mchezaji mzuri, wa ajabu-siku inayofuata, mimi na (Mkurugenzi wa Chelsea) bwana Mrs Granovskaia na (mkurugenzi wa ufundi) Michael Emenalo tutagongewa milango na wachezaji wakisema inawezekanaje tumeichezea klabu mechi 200 na kushinda hili na lile, lakini bwana mdogo anatuzidi mshahara?
“Inawezekanaje kijana wa miaka 19 anakuja hapa na kupata hela ambazo hata mimi sipati? ningeua usawa wa timu na nisingeruhusu hilo kutokea”.
‘Filipe Luis aliichezea Brazil, ameshinda makombe ya Ulaya, alicheza nusu fainali ya UEFA, huyu mchezaji ni bei rahisi kuliko huyu mtoto wa England?
“Sikosoi klabu nyingine kwa kumlipa vile. Lakini kwa klabu yangu, tunaweza kusema ingekuwa mbaya kwetu”.