Salamu: Van Gaal (katikati) amekutana na msaidizi wake Ryan Giggs (kushoto) na makamu mwenyekiti Ed Woodward.
KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Carrington leo jumatano kuanza kazi yake mpya.
Mholanzi huyo alipigwa picha akiwa geti kubwa, lakini baadaye klabu iliposti picha katika mtandao wake wa Twita akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward.
Van Gaal alitaka kuonana na wachezaji wake baada ya kombe la dunia pamoja na viongozi wa klabu hiyo.
Van Gaal ametua kazini siku nne tu tangu aiongoze Uholanzi kushika nafasi ya tatu na kwa maana hiyo amejinyima mapumziko.
Kocha huyo mwenye miaka 62, ni kocha wa kwanza kuiongoza Man United kutoka nje ya British,na hatakuwa na muda wa kupoteza katika harakati zake za kuijengga United.
Kesho alhamisi, atatangazwa rasmi katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari ya kwenda nchini Marekani kuweka kambi ya maandilizi ya kabla ya msimu.
United itacheza mechi dhidi ya Los Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na Real Madrid, wakati mechi ya kwanza ya Van Gaal katika dimba la Old Trafford itakuwa ya kirafiki dhidi ya Valencia Agosti 12 mwaka huu.
Siku nne baadaye United wataanza ligi kuu kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Swansea.