CHELSEA imethibitisha kukamilisha usajili wa Diego Costa kwa kumsainisha mkataba wa miaka mitano katika dimba la Stamforf Bridge.
Dili la kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispani lilikubaliwa rasmi julai mosi, lakini mshambuliaji huyo wa kati amekamilisha kila kitu na kuwa mchezaji wa Blues leo hii.
Jose Mourinho ameilipa Atletico Madrid paundi milioni 35 ikiwemo ada ya wakala.
Costa aliweka wazi sababu ya kujiunga na The Blues mwezi juni mwaka huu, akieleza kuwa amefurahi kujiunga na moja ya klabu kubwa zaidi duniani.
Nyota huyo mwenye miaka 25 amesaini mkataba Stamford Bridge ambao utamfanya alipwe kiasi cha paundi laki mbili na nusu kwa wiki.