Kwenu, Madridisno,
Maisha yangu Real Madrid yamefikia mwisho. Ni ngumu kuandika yale yote niliyopitia katika mistari michache, lakini nataka barua hii ifikishe ujumbe wa kila ninachojisikia wakati huu wa kuagana. Katika hii miaka minne nimepata heshima ya kuvaa jezi hii, hakuna ninachojisikia zaidi ya kujivunia kwa kile nilichopitia na kufanikiwa pamoja na wenzangu.
Bahati mbaya leo nalazimika kuondoka, lakini nataka kuweka hili wazi haikuwa nia yangu. Kama mtu yeyote anayefanya kazi siku zote anataka kusonga mbele. Baada ya kushinda ‘ La Decima’ nilienda katika kombe la dunia nikiwa na matumaini ya kupata mkataba mpya ambao haukuja. Mambo mengi na uongo mwingi ulizungumzwa. Siku zote walitaka kuanzisha kitu ili mimi niondoke klabuni, lakini sikufanya hivyo.
Kitu pekee nilichoomba ni kile ambacho kingekuwa haki. Kuna vitu vingi navithamini na vingi kati ya hivyo haviusiani kabisa na mshahara wangu. Ninamatumaini nitasonga mbele. Manchester United ni moja ya klabu kubwa duniani ambako ninataka kutengeneza historia. Nimekuwa na bahati sana ya kutumia chumba kimoja cha kubadilishia nguo na wachezaji wazuri sana, ambao wamekuwa marafiki wa kweli. Nadhani huo ndiyo ulikuwa ufunguo wa La Decima.
Napenda kuomba radhi kutokana na kipindi nilichokosea uwanjani na nje ya uwanja. Haikuwa nia yangu kuumiza mtu yeyote. Nilitoka jasho kwa ajili ya jezi hii katika kila mechi nilidhani ilikuwa ni ya mwisho. Kulikuwa na wakati mambo yalikuwa sawa kwangu kuliko kwa wengine, lakini nachoweza kusema ni kuwa mara zote nilijitoa kwa uwezo wangu wote.
Nataka kuishukuru Hispania kwa kila kitu ilichonipa na hasa hasa kuruhusu mwanangu kuzaliwa katika dunia hii. Na kwa watu muhimu sana wa hospitali ya Monteprincipe, ambayo siku zote itakuwa moyoni mwangu. Mke wangu, mwanangu na mimi siku zote tutaendelea kushukuru. Pia kwa wachezaji wenzangu ambao walinipa sapoti siku zote kwenye wakati mzuri na mbaya. Kwa watu wa ufundi nilifanya nao kazi na kwa wote wanaofanya kazi siku klabuni ambao ninatumaini nitaendelea kuwa na uhusiano nao mzuri daima.
Natumaini Real Madrid watakuwa na msimu mzuri sana na kupata mafanikio ambayo klabu hii siku zote imekuwa ikiyatafuta. Siku zote nitakumbuka muda ule kwenye Supercopa niliponyanyuka pale Bernabeu na nikapata upendo wa kweli kutoka kwa mashabiki. Asanteni sana. Nilifurahi sana na sikuwa na njia nyingine ya kuwaaga katika mechi ile ambayo bahati mbaya ilikuwa mechi yangu ya mwisho.
Hala Madrid! Milele -