MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ atatoa burudani ya kufa mtu katika tamasha la ‘Simba Day’ linalotarajia kufanyika kesho kutwa (Agosti 9 mwaka huu) katika uwanja wa Taifa, uliopo Chang`ombe jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amezunguma na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa JB Belmont katikati ya jiji na kueleza kuwa saabu ya kumchagua Diamond ni kutokana na ukweli kuwa ndiye msanii anayetamba kwa sasa.
Daimond ambaye kwasasa ‘anasumbua’ na wimbo wa My Number One na Mdogo mdogo ataungana na bendi ya Twanga Pepeta na wasanii wengine kama vile Dully Sykesm, Barnaba, Mataalum na makundi ya kudansi kutumbuiza katika tamasha hilo la kila mwaka.
Mbali na burudani hizo, kutakuwa na mechi mbili za mpira wa miguuu ambapo timu ya vijana ya Simba chini ya miaka 20 itachuana na timu ya vijana ya Azam fc.
Baadaye kikosi kamili cha Simba kitaoneshana kazi na Zesco United ya Zambia.
Katika mechi hiyo, Simba imeahidi kutumia kikosi chake kamili ambapo wachezaji wote waliowasajili majira haya ya kiangazi mwaka huu wataonekana katika mechi hiyo maalum ya kuwatambulisha kwa mashabiki wao.
“Wachezaji wote wataonekana siku hiyo na mshambuliaji wetu mpya kutoka kenye Kiongera tayari amewasili nchini”. Alisema Kaburu.
Naye meneja wa Zesco, Mavuto alitamba kuwafunga Simba katika mechi ya kesho ingawa hana uhakika watawafunga magoli mangapi, lakini alisisitiza kuwa watafanya vizuri, hivyo kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho.