Nyota anayewidnwa: Mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao (kushoto) anawindwa na klabu za Real Madrid na Liverpool majira haya ya kiangazi.
REAL Madrid wamepewa nafasi kubwa ya kumsajili Radamel Falcao ukilinganisha na timu ya Liverpool anayoiwinda saini ya nyota huyo.
Liverpool wameamua kumwendea mshambuliaji huyo wa Manaco baada ya kushindwa kumsajili Wilfried Bony wa Swansea na kushindwa kumnasa mshambuliaji wa QPR, Loic Remy kutokana na kushindwa kufuzu vipimo vya afya.