Dili limetiki: Frank Lampard amejiunga na Man City kwa mkopo.
MANCHESTER City wamethibitisha kumsajili kiungo wa zamani wa Chelsea, Frank James Lampard kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita.
Mabingwa hao wa England wametangaza taarifa hizo leo asubuhi na Lampard atafanya mazoezi na wachezaji wenzake jioni ya leo.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 amejiunga na Manchester City kwa uhamisho huru kutokea klabu dada na Man City ya New York City, na amerudi England kwasababu ligi ya Marekani haijaanza mpaka mwezi machi mwakani.
Lampard atavaa jezi namba 18 katika dimba la Etihad, na hiyo ni namba yake ya zamani aliyokuwa anavaa katika klabu yake ya zamani ya West Ham.
Kiungo huyo ataichezea Man City katika mechi za ligi kuu na michuano ya Ulaya.
Kiungo huyo aliiambia tovuti rasmi ya klabu kuwa: ‘Kujiunga na Manchester City ni nafasi ya ajabu kwangu kuendelea kufanya mazoezi na kucheza soka la kiwango cha juu na nina uhakika itanisaidia kabla ya kwenda New York City’