Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto kwake ni Kocha Mkuu Marcio Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto
Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
“Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza” alisema Beno.
Lakini katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu “aliongeza Beno.”
Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.
Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC .
Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.
Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.
Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifaa