Kiongozi: Louis van Gaal alisema mtazamo wa Wayne Rooney ndio sababu ya kumteua kuwa nahodha.
LOUIS van Gaal amesifu mtazamo wa Wayne Rooney na kuamua kumteua kuwa nahodha wa Manchester United, lakini amemuonya kujiheshimu nje na ndani ya uwanja.
Mholanzi aliweka wazi kuwa alizungumza na Roonye kuhusu kumvalisha kitambaa cha umeneja baada ya mechi ya jumanne usiku dhidi ya Valencia kufuatia mshambuliaji huyo kujituma zaidi kuwa kiongozi.
Bosi wa United alisema: “Nimempa unahodha kwasababu ya mtazamo wake uwanjani na kwenye uwanja wa mazoezi.”
“Sio nje ya uwanja sana, lakini nimemuambia kuwa yeye ni muhimu sana kwangu na amekubali majukumu yake.
“Nilipenda sana jinsi alivyofanya mazoezi na kiwango chake na namna alivyowaongoza wenzake.
“Tukiwa Marekani alifunga magoli mengi na kutoa pasi za mwisho nyingi. Huyu ndiye Wayne ninayemhitaji”.
Akizungumza kuelekea mechi ya kwanza ya Manchester United dhidi ya Swansea kesho jumamosi, Van Gaal pia alithibitisha kuwa Robin van Persie hana nafasi ya kucheza.
Aliongeza kuwa Luke Shaw hatacheza mechi hiyo baada ya kuumia na atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne.