Mashindano ya Castle Lager Perfect 6 ambayo yalifanyika nchi nzima katika muda wa miezi mitatu yatafikia tamati wikendi hii katika fainali ambazo zitachezwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam tarehe 16 Agosti, 2014 ambapo kiingilio itakuwa ni bure. Washindi wa fainali hizo zinazosubiriwa kwa hamu watatembelea uwanja wa Camp Nou na kuishuhudia timu ya FC Barcelona ikicheza laivu na safari hiyo itagharamiwa kila kitu na Castle Lager.
Meneja wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo amesema leo kwamba Fainali za Castle Lager Perfect 6 zitahusisha timu nane ambazo zilishindana kwenye kanda sita za nchi wakati wa mashindano hayo ikiwemo timu ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA).
“Timu zitakazoshiriki kwenye fainali za Castle Lager Perfect 6 ni pamoja na Pile United (Temeke), Barafu FC (Ilala), Infinity Communications (Kinondoni), Musoma Veterans (Musoma), Kitayosa FC (Arusha), Schalke 04 (Morogoro), Green City (Mbeya), na TASWA FC (Vyombo vya Habari).”

Nshimo alisema “Timu itakayoshinda fainali hizo itakuwa pia imeshinda nafasi ya aina yake kwenda Hispania kutembelea uwanja mkubwa zaidi barani Ulaya wa Camp Nou unaomilikiwa na FC Barcelona. Timu hiyo itaweza kujionea vivutio mbalimbali huko Camp Nou na kuishuhudia FC Barcelona ikicheza mechi laivu kwenye uwanja huo maarufu.”
Nshimo aliongeza kuwa mambo yote yatakuwa Leaders Club wikendi hii ambapo fainali hizo zitasindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa msanii maarufu wa muziki wa dansi Ali Choki mbaye ni kati ya waimbaji bora nchini pamoja na bendi yake ya Extra Bongo. “Ali Choki ataburudisha wachezaji pamoja na watazamaji kwa nyimbo zake mbalimbali zinazopendwa katika tukio hili ambalo linatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.” Ili kuhakikisha wachezaji na mashabiki wanaburudika kutakuwepo na viburudisho na Nyama Choma wakati michezo ikiendelea.

Pia Nshimo alisema kwamba, droo kubwa ya kampeni ya SMS ya iliyoenda sambamba na mashindano ya Castle Lager Perfect 6 itafanyika siku hiyo na kupata washindi ambao wataandamana na timu itakayoshinda kwenda Camp Nou.
Mashindano ya Castle Lager Perfect 6 Tournament yalizinduliwa mwezi Aprili mwaka huu Six yakiwa yamelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza mpira wa miguu, kuleta pamoja wanywaji wa Castle Lager ili wafurahie pamoja na kuwapa zawadi wateja wa bia hiyo.