1407530992465_wps_1_Mikel_Arteta_of_Arsenal_i
Anapanda cheo: Mikel Arteta, ambaye kwa sasa ni nahodha msaidizi wa Asernal anatarajiwa kupandishwa na kuwa nahodha.
ARSENE Wenger anatarajia kumteua Mikel Arteta kuwa nahodha wa klabu ya Arsenal kufuatia maamuzi ya kumuuza
 Thomas Vermaelen.
Bosi huyo wa Gunners , ambaye amepangwa dhidi ya klabu yenye mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba, Besiktas katika michezo ya mtoano ya UEFA, anahitaji nahodha kufuatia kuondoka kwa Vermaelen kwenda Barcelona.
Anerta ambaye kwa sasa ni nahodha msaidizi anapewa nafasi kubwa ya kuchukua beji hilo. 
Pia Per Mertesacker anapewa nafasi kubwa na Wenger ya kuwa nahodha msaidizi.
Vermaelen alikuwa nahodha msaidizi wakati nahodha Robin van Persie anaondoka mwaka 2012.
Hatima ya baadaye ya Arteta bado haifahamiki sana ukizingatia amebakiwa na miezi 12 tu katika mkataba wake, lakini mazungumzo ya kuongeza yanaendelea.
Asernal watacheza mechi yao ya kwanza nchini Uturuki, Agosti 19 kabla ya kucheza mechi ya marudiano katika dimba la Emirates siku nane baadaye.
Wearing the armband: Mikel Arteta stepped in as captain last season
Moving on: After being strongly linked with Manchester United, Thomas Vermaelen is now off to Barcelona

 
Top