MARCOS Rojo amethibitisha kukamilisha usajili wake kujiunga na Manchester United akitokea klabu ya Sporting Lisbon na kusisitiza kuwa ndoto ya kucheza ligi kuu Egland imetimia.
Inafahamika kuwa mashetani wekundu wamekubali kutoa paundi milioni 20 ili kumnasa Muargentina huyo, huku Luis Nani akijiunga kwa mkopo katika misingi mingine.
“Nahisi kama ni ndoto kuwa mchezaji wa Manchester United,” Beki huyo aliwaambia ARV Radio Continental. “Kuondoka Sporting Lisbon haikuwa rahisi”.
Siku chache zilizopita Rojo alitawala kwenye vyombo vya habari baada ya kuondoka katika mazoezi ya Sporting kufuatia klabu hiyo kukataa ofa ya United, lakini aliwaomba radhi wachezaji na mashabiki kwa kitendo hicho kisichokuwa cha kiungwana.
Beki huyo mwenye miaka 24 alifika fainali ya kombe la dunia akiwa na nchi yake ya Argentina na kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani