Wojciech Szczesny wa Arsenal akifungwa bao na Martin Demichelis wa Manchester City katika dakika ya 83.
MARTIN Demichelis ameiokoa Manchester City dhidi ya Arsenal baada ya kusawazisha bao la pili kwa kichwa na kulazimisha sare ya mabao 2-2 katika dimba la Emirates.
Arsenal walimuanzisha mshambuliaji wao mpya, Danny Welbeck ambaye almanusura afunge bao katika dakika ya 11, lakini mpira wake uligonga mwamba.
Sergio Aguero ndiye alivunja ngoma ya Arsenal na kufunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza.
Mabao ya kipindi cha pili ya Jack Wilshere na Alexis Sanchez yaliwapa Arsenal matumaini ya kuibuka na pointi tatu muhimu, kabla ya Demichelis kusawazisha katika dakika ya 83.
Kocha wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger amezidi kukumbwa na balaa na leo hii beki wake Mathieu Debuchy aliteguka mguu na kutolewa nje ya uwanja kwa machela.