Nimekuandikia hiyo sentensi hapo juu nikiweka kumbukumbu vizuri wakati huu ambapo imebaki miezi miwili kufanyika kwa show ya Jose Chameleone wa Uganda ambae amepanga kuifanya show yake mwenyewe nchini kwao December hii huku kiingilio kikiwa ni zaidi ya laki sita za Tanzania ambazo ni shilingi milioni moja za Uganda.
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Jose Chameleone amesema >>> ‘nachekelea watu ambao wanasema Milioni? nani atampa hiyo milioni? watu wengi wanauliza mbona milioni moja? msanii mmoja? kuna watu ambao hawajapata bahati ya kumuona Chameleone akiwa anafanya mazuri yake, kuna matajiri flani wanataka kuja kwenye show yangu lakini wanaogopa wakija kuna cameraman wengi wanawasumbua na vitu kama hivyo’
- ‘Sio eti nimetaka kujipandisha bei lakini nataka kuwajali pia wale ambao hawawezi kunitembelea kwenye show za kawaida, najua watu wanashangaa na kuuliza mbona milioni?? …….sio sababu wewe au mimi hatuna milioni ndio wote hatuna milioni, kuna watu ambao milioni ni kama elfu moja, elfu kumi au laki moja’
- ‘Usiulize wanaotengeneza Benz mbona wanauza bei kubwa zaidi ya Toyota, kama huna hela ya Benz nunua Toyota, sio kwa ubaya lakini nataka nijali watu wote.. hii ni kwa wale wasioweza kuja kwenye show za elfu 10 na elfu 20, na wao wapate wakati wao…. hii hela ni kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Karamoja wanaoishi kwenye maisha duni
- 'pia ninjia ya kuweza kuonyesha msani wa East africa anasamani kubwa pia akiamua kujipa thamani anayo ya ukubwa anayo iitaji.