Mbrazil,
Andrey Coutinho (katikati) aliinyoa Prisons goli moja katika ushindi wa Yanga
wa 2-1 uwanja wa Taifa
Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
LIGI
kuu soka Tanzania bara msimu huu inaonekana kuwa na changamoto tangu mapema.
Mpaka
sasa zimechezwa raundi mbili, lakini timu zimenyoana si mchezo. Hebu
nikukumbushe namna zilivyonyoa, zilivyonyolewa na kunyoana.
Stand
United ikitokea kunyolewa 4-1 na Ndanda fc uwanja wa Kambarage Shinyanga nayo
ilimnyoa Mgambo JKT 1-0 uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.
Prisons
ikitokea kuinyoa Ruvu Shooting 2-0 uwanja wa Mabatini, Pwani nayo jana
ilinyolewa 2-1 na Yanga.
Yanga
akitokea kunyolewa 2-0 na Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri Morogoro, ilifanikiwa
kuinyoa Prisons jana uwanja wa Taifa.
Kagera
Sugar ikitoka kunyolewa 1-0 na Mgambo JKT mechi ya ufunguzi Mkwakwani Tanga,
nayo iliinyoa JKT Ruvu 2-0 jana, Azam Complex, Chamazi.
Coastal
Union ikitokea kunyoana 2-2 na Simba, ilinyolewa 1-0 na Mbeya City iliyoshindwa
kunyoana na JKT Ruvu mechi ya ufunguzi.
Polisi
Morogoro ikitokea kunyolewa 3-1 na Azam fc uwanja wa Azam Complex Chamazi,
ilinyoana 1-1 na Simba jumamosi iliyopita uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Ndanda
fc iliyotoka kuinyoa Stand United 4-1 uwanja wa Kambarage Shinyanga, nayo
ilinyolewa 3-1 na Mtibwa Sugar uwanja wa Manungu, Complex.
Ruvu
Shooting yenyewe imenyolewa mara mbili( 2-0 kutoka Prisons, 2-0 dhidi ya Azam
fc).
Timu
pekee ambazo zina wembe mkali ni Mtibwa Sugar na Azam fc.
Mtibwa
Sugar wamezinyoa timu mbili. Waliinyoa Yanga 2-0 na wikiendi iliyopita
wakainyoa Ndanda fc 3-1.
Azam
fc nao wamezinyoa timu mbili. Waliinyoa Polisi Morogoro 3-1 na juzi wameinyoa
2-0 Ruvu Shootings.
Ngoja
tusubiri kama timu zitaendelea kunyoa, kunyolewa na kunyoana kwa staili hii….