Reus ruled out for a month
Nje: Reus akiugulia maamuzi katika  mechi ya jana usiku dhidi ya Scotland 
NYOTA wa Borussia Dortmund, Marco Reus ataikosa mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Arsenal huko Westfalenstadion kufuatia kuvunjika mfupa wa kifundo cha mguu katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Scotland.
Mkali huyo wa Ujerumani atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne baada ya kukatwa buti na Charlie Mulgrew jana usiku.
Arsenal watasafiri kwenda Ujerumani Septemba 16 mwaka huu kukabiliana na Dortmund katika mechi ya makundi ya ligi ya mabingwa-kwa mara ya nne ndani ya miaka minne ambapo klabu hizo zinapangwa kundi moja na Reus atarudi uwanjani mpaka mapema mwezi oktoba.


 
Top