1410716455823_wps_11_Mata_and_Di_Maria
Mhispania Juan Mata alimtafsiria kiingereza Angel di Maria katika mahojiano ya baada ya mechi.
ANGEL di Maria amesema bao lake la  kwanza aliloifungia Manchester United jana katika mchezo wa nyumbani linaweza kuonekana kama alibahatisha, lakini Muargentina huyo amedai alipanga apige hivyo.
Bao  la kwanza la Di Maria katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR alifunga kwa mpira wa adhabu ndogo, mita 35 kutoka kwenye golini.
Mata presents Di Maria with his Man of the Match award in the Old Trafford tunnel
Di Maria aliyesajiliwa kwa paundi milioni 60 majira ya kiangazi mwaka huu akitokea Real Madrid, amesema goli hilo limetokana na mazoezi aliyofanya.
“Nina furaha sana ya kufunga goli langu la kwanza nyumbani,” alisema Di Maria.”Tumekuwa tukifanya mazoezi kwa wiki nzima na nilifunga kama vile, sio ajabu kwangu”

 
Top