Suarez to Barcelona and the 10 most expensive transfers of the summer
Nyota wa FC Barcelona, Luis Suarez akiwa ameshika jezi yaa mkutano na waandishi wa habari wakati akitambulishwa katalunya.
DIRISHA la usajili ni jambo muhimu sana katika maisha ya wachezaji duniani. Wachezaji mbalimbali wanavuna hela nyingi wakati wa usajili, lakini mpaka siku ya mwisho kuna baadhi ya wachezaji wanashindwa kufikia ndoto zao.
Hapa chini ni orodha ya wachezaji waliouelezea usajili wa dirisha la majira ya kiangazi  kwa namna ya kutimiza ndoto zao.
Marcos Rojo (Sporting Lisbon kwenda Man United): “Ilikuwa ndoto kucheza Manchester United. Ni ndoto kuwasili Manchester.”
Mehdi Benatia (Roma kwenda Bayern Munich): “Bayern ina wachezaji wengi wakubwa. Wana kikosi imara na ni ndoto kuwa sehemu yao.
Chicharito (Man United kwenda Real Madrid): “Kwa upande wangu ndoto imekuwa kweli.
Danny Welbeck (Man United kwenda Arsenal): “Niliota kuichezea timu hii kabla. Kwangu mimi hatimaye imetokea.”
Divock Origi (Lille kwenda Liverpool): “Kwangu mimi ilikuwa ndoto kucheza klabu kubwa. Najua Liverpool ni klabu yenye historia kubwa, kwahiyo kwangu mimi imekamilika.”
Dejan Lovren (Southampton kwenda Liverpool): “Ndoto imekuwa kweli.
Filipe Luis (Atletico Madrid kwenda Chelsea): “nikiwa mtoto nilikuwa na ndoto ya kucheza ligi kuu England siku moja, kwahiyo Chelsea walipokuja, kwangu mimi yalikuwa maamuzi rahisi.”
James Rodriguez (Monaco kwenda Real Madrid): “Ni jambo la ajabu kusikia klabu kubwa kama Real Madrid imevutiwa na mimi. Ilikuwa ndoto kusajiliwa na  klabu ya ndoto zangu.”
Luis Suarez (Liverpool kwenda Barcelona): “Siwezi kuamini kama ndoto nzuri kama hii imetimia.”
Rickie Lambert (Southampton kwenda Liverpool): “Siku zote nilikuwa na ndoto ya kuichezea Liverpool, lakini nilidhani nafasi ya kuichezea imekwisha. Sikuwahi kuwaza kama nafasi itarejea.”
Ander Herrera (Athletic Bilbao kwenda Manchester United): “Kujiunga na Manchester United ni ndoto iliyokuwa kweli.”
Ivan Rakitic (Sevilla kwenda Barcelona): “Ndoto imekuwa kweli.
Lakini inaonekana kwa wachezaji fulani walikuwa na ndoto tofauti. Falcao alitweet kuwa ndoto ingetimia kama angesajiliwa na Real Madrod  badala yake alijiunga na Manchester United ambapo alitangaza kama ndoto imekuwa kweli.
Nini tunajifunza hapa? ni kwamba dirisha la usajili majira ya kiangazi limekamilisha ndoto za wachezaji wengi walizokuwa nazo tangu utotoni.

 
Top