Oscar Pistorius akiwasili katika mahakama ya Pretoria leo mchana kusikiliza keshi inayomkalibi
JAJI anayeendesha kesi ya mauaji inayomhusu mwanariadha wa Afrika kusini, Oscar Pistorius, hajamkuta na hatia ya kumuua kwa kukusudia mpenzi wake, mwanariadha wa Olympic, Reeva Steenkamp
Katika kesi hiyo iliyosikilizwa leo, Jaji Thokozile Masipa alisema ushahidi wa kuthibitisha kuwa Pistorius, 27 aliua kwa makusudi haujajitosheleza kutoka kwa mwendesha mashitaka.
“Ushahidi wa kuhusika na mauaji, huo umejitosheleza” alisema Jaji, lakini hakutoa hukumu juu ya kesi hiyo ya Pistorius na kutoa wito kwa ajili ya chakula cha mchana mahakamani hapo.
Mbivu na mbichi zitajulikana leo hii.
Hata kama Pistorius hatakutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia, bado anaweza kwenda jela kwa kosa la kumuua Steenkamp.
Mwanaridha huyo alikiri kutenda kosa hilo, lakini alisema hakukusudia.
Mashahidi wa utetezi walidai kuwa Pistorius alimuua kwa makusudi mpenzi wake kutokana na ugomvi uliotokea baina yao na majirani walisikia.