Anataka zaidi? Paul Pogba (kulia) atalipwa paundi elfu 23 kwa wiki kwa wakati huu katika klabu yake ya Juventus
LIGI ya Italia imeshuka umaarufu wake ukilinganisha na ligi nyingine za ulaya na hii inatokana na mishara ya wachezaji wa Seria A iliyotangazwa jumatatu ya wiki hii.
Daniele de Rossi ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ambapo anachukua paundi laki moja kwa wiki na Gonzalo Higuain anamfuatia kwa kulamba paundi elfu 84 kwa wiki na wa tatu ni Carlos Tevez anayepokea paundi elfu 70 kwa wiki.
Kwa mujibu wa gazeti la Gazzetta dello Sport, klabu za Serie A kwa sasa zinatumia karibia paundi milioni 500 kwa ajili ya malipo ya mishahara wa wachezaji chini ya kiwango cha mwaka 2011 na wachezaji wanaolipwa zaidi wanachukua hela ndogo ukilinganisha na wachezaji nyota wa ligi kuu England na La Liga.
Kwa mfano, Paul Pogba, anapokea paundi elfu 23 kwa wiki msimu huu licha ya kuwa miongoni mwa vijana wenye kiwango cha juu duniani na katika klabu yake ya Juventus.
Juventus, ndio klabu inayoongoza kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya mishara na ni klabu pekee ya Italia ambayo inaongeza mishahara ya wachezaji kutoka 2013/2014 ambapo Carlos Tevez na Arturo Vidal sasa wanapokea zaidi ya paundi elfu 60 kwa wiki.
Nyota wa Roma, Daniele De Rossi ndiye analamba mkwanja mrefu katika mkataba wake wenye thamani ya paundi milioni 5.2 bila kujumuisha posho.
Nyota wa zamani wa Cheslea na sasa Roma Ashley Cole aliamua kwenda Italia baada ya kutoongezewa mkataba Chelsea na amesaini mkataba atakaomfanya apokee paundi elfu 35 kwa wiki katika kikosi hicho cha Rudi Garcia.