Frank
Lampard akishangilia goli lake la tatu katika mechi mbili dhidi ya
Sheffield jana
SHREWSBURY
Town, timu pekee ya daraja la chini zaidi iliyosalia katika michuano ya kombe
la ligi ‘Capital One Cup’ amepangwa kukutana na timu ngumu ya ligi kuu ya
England, Chelsea kwenye mechi ya raundi ya nne.
Raundi
iliyopita Shrews inayocheza daraja la pili iliwaondoa mabingwa wa Championship,
Norwich na sasa itawakaribisha Chelsea walioshinda 2-1 dhidi ya Bolton
jana usiku.
Mabingwa
watetezi, Manchester City, walioitoa Sheffield jana kwa kuifunga mabao 7-0
katika dimba la Etihad watachuana na Newcastle inayocheza ligi kuu.
Liverpool
waliosonga mbele kwa penati 14-13 dhidi ya Middlesbrough jumanne usiku,
watachuana na Swansea City, zote zinacheza ligi kuu.
Stoke
wataikaribisha Southampton , wakati Tottenham watakuwa nyumbani dhidi ya
Brighton.
Mechi
nyingine za raundi ya nne zitawakutanisha Sheffield United watakaosafiri
kuifuata MK Dons na Fulham watakabiliana na Derby.
Capital
One Cup: MECHI ZA RAUNDI YA NNE
Tottenham
Hotspur vs Brighton
Stoke
vs Southampton
Bournemouth
vs West Brom
Shrewsbury
vs Chelsea
Liverpool
vs Swansea
MK
Dons vs Sheffield United
Manchester
City vs Newcastle United