Simba SC itacheza na mahasimu wao Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika michezo mitatu iliyopita Simba haijapata ushindi, huku mahasimu wao wakiwa na pointi sita katika nafasi ya tatu ya msimamo. Yanga ni timu iliyokamilika kwa sasa, kwa maana ya kucheza kitimu, umoja na ushirikiano.
Kabla ya safari ya Afrika Kusini, kikosi cha Simba kimeonekana kukosa ‘ utimamu wa mwili na akili’ kwa maana ya wachezaji wake kucheza mpira huku wakiwa na mambo yanayowasumbua, umoja, kiwango cha chini kutoka kwa baadhi ya wachezaji, majeraha, na ufiti wa mchezaji mmoja mmoja, kikosi cha Patrick Phiri kimekuwa katika ‘ majanga’ hayo, lakini kama, mwalimu hapaswi kutumia sababu hizo kufungwa na mahasimu wao ambao wanaingia katika mchezo wa tano mfululizo wakiwa katika ‘ umbo zuri’.
Mwaka mmoja uliopita, Kiemba alikuwa mchezaji bora zaidi katika kikosi cha kocha Kim Poulsen, lakini ghafla kiwango cha mchezaji huyo kiliporomoka kiasi cha kupoteza nafasi yake hadi katika klabu yake. Mwalimu, Nooij ameendelea kumuita kiungo huyo mzoefu na Kiemba mwenye miaka 31 hivi sasa aliweza kuthibitisha kuwa yuko safi baada ya kufunga huku akiichezesha timu. Nooij alimpanga kiungo huyo kama mchezesha timu mkuu akitokea katikati ya uwanja.
Alicheza kwa dakika 67 huku akiwa makini, mtulivu na kupiga pasi zilizofika kwa walengwa, zaidi alikuwa akikimbia uwanjani tofauti na ilivyozoeleka. Stars ilicheza huku wachezaji wake wakikimbia na jambo hilo liliupendezesha mchezo wa Kiemba ambaye aliweza kupiga pasi nyingi kuelekea
Marcio Maximo kocha wa Yanga anaitegemea zaidi safu yake ya kiungo katika kushambulia na kujihami, lakini, Phiri hajui mahala kwa kushikilia hadi sasa. Kati ya mambo yanayomuumiza kichwa kocha huyo ni kumkosa kiungo mshambulizi, Paul Kiongera, lakini bado Phiri anaweza kurudia rudia mara kadhaa video ya mchezo wa jana kati ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Benin anaweza kupata sehemu ya kuanzia.
Achana na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na Haroun Chanongo katika mchezo wa jana, kiungo wa mashambulizi, Amri Kiemba alikuwa katika ubora wa juu. Je, kiwango cha Kiemba dhidi ya Benin kilikuwa na maana gani?. Anapokuwa fiti kimwili na kiakili, Kiemba ni mmoja wa viungo bora zaidi wachezesha timu wa Kitanzania, lakini ameshuka kiwango katika kipindi cha miezi ya karibu kabla ya kiwango cha aina yake hapo jana.
Phiri atakuwa na furaha sasa kwa sababu mechi kati ya timu hizo kubwa nchini huwa inahitaji wachezaji wazoefu walio fiti. Kiemba ameonesha kukimbia bila maumivu, ameonyesha ni mchezaji mzoefu mwenye nguvu, akili ya mpira, na mfungaji wa mechi ‘ maalumu’.
Kiwango chake ni kama kimefikisha ujumbe kwa mwalimu wake kuwa anaweza kufanya vizuri akicheza na Piere Kwizera, Shaaban Kisiga, Said Ndemla, Jonas Mkude au mchezaji yeyote Yule ambaye atapaswa kucheza naye.