MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Mbeya City ambao hawajafungwa hata goli moja msimu huu, timu hizo zitakapovaana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya keshokutwa.
Azam, ambao mpaka sasa wamecheza mechi 37 za VPL bila kufungwa; nane za msimu wa 2012/13, 26 za msimu uliopita na tatu za msimu huu, watashuka kwenye uwanja huo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi mgumu wa 2-1 dhidi ya ‘wababe’ hao, ushindi ambao uliwapa ubingwa wa VPL Machi 23, mwaka jana wakiwa mechi moja mkononi.
Joseph Omog, Kocha wa Azam FC, amesema kikosi chake kilichotua mjini Mbeya juzi, kiko tayari kwa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wakazi wengi wa Jiji la Mbeya.
Amesema mazoezi ya ufukweni ambayo timu yake imeyafanya jijini Dar es Salaam mara tu baada ya mechi yake yao iliyomalizika kwa suluhu dhidi ya Tanzania Prisons, yanampa matumaini timu yake kuibuika na ushindi katika mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na historia ya timu hizo.
Kocha Juma Mwambusi wa Mbeya City amesema kikosi chake ambacho kiko mafichoni kuwawinda ‘wanalambalamba’, kiko tayari kulipa kisasi cha kufungwa katika mechi iliyopita.
Azam FC, ni timu pekee ya VPL iliyoifunga Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine msimu uliopita, ikiwa ni kipigo cha tatu na cha mwisho kwa timu hiyo msimu mzima ikifungwa pia na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaamkabla ya kupoteza kwa mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara, Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Hakuna timu nyingine ya nje ya mkoa wa Mbeya zaidi ya Azam FC na Oljoro JKT iliyopata ushindi kwenye Uwanja wa Sokoine msimu uliopita. Oljoro iliyoporomoka daraja, iliifunga Tanzania Prisons mzunguko wa kwanza.

Aidha, Azam FC na Mbeya City ndiyo timu pekee zilizomaliza mzunguko wa kwanza wa VPL msimu uliopita bila kupoteza mechi hata moja, zikitoka sare ya mabao matatu zilipokutana kwenye Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam huku mshambuliaji Mwegane Yeya wa City akiandika historia mpya katika soka la Tanzania kwa kufunga ‘hat-trick’ ya vichwa.
Mbali na kusaka kisasi cha kufungwa katika mechi iliyopita, Mbeya City wataingia uwanjani wakisaka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC baada ya kucheza mechi 37 bila kufungwa na pia kutwaa taji la VPL bila kupoteza mechi hata moja wakati matajiri wa Dar es Salaam watakuwa wakisaka ubabe kwa kuwa timu pekee iliyoifunga Mbeya City mara mbili kwenye uwanja wake wa nyumbani bila timu nyingine za VPL kufanya hivyo.
Azam wanahitaji pia kuilinda hadhi yao ya kutofungwa katika mechi 38 za ligi kuu na kuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya timu hiyo ya Manispaa ya Jiji la Mbeya.
Azam FC iliyofungwa goli moja msimu huu ikiwa imefunga magoli matano huku mshambuliaji wake Mrundi Didier Kavumbagu akifunga magoli manne, iko nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi saba, mbili nyuma ya vinara, Mtibwa Sugar ambao kesho watashuka kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kumenyana na ‘maafande’ wa Polisi Morogoro.
Mbeya City iko nafasi ya nne ikiwa na pointi tano ikiwa imeshinda mechi moja dhidi ya Coastal Union na kutoka suluhu dhidi ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting. Timu hiyo ya kocha Mwambusi haijaruhusu nyavu zake kutikishwa huku safu yake ya ushambuliaji ikionekana ni butu msimu huu kwani wamefunga goli moja tu, tena kwa penalti katika mechi zote tatu za mwanzo.
Hata hivyo, macho na masikio ya wengi keshokutwa yataelekezwa Uwanja wa Taifa katika pambano la kwanza la watani wa jadi msimu huu, Simba, waliokuwa kambini Afrika Kusini, wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kutoka sare tatu mfulizo katika mechi zote tatu za mwanzo.
Vita nyingine ya VPL wikendi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara wakati wenyeji Ndanda FC watakapowakaribisha maafande wa Ruvu Shooting walio mkiani mwa msimamo wakiwa hawajafunga hata goli moja wakipoteza mechi mbili za mwabnzo kabla ya kutoka suluhu na Mbeya City.
Stand United watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba mjini Bukoba, Kagera wakati Coastal watavaana na majirani zao Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Jumapili kutakuwa na mechi moja itakayozikutanisha Tanzania Prisons na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Sokoine.