“
Kazi ya pamoja(Teamwork) inaleta matokeo mazuri, lakini maono hayo huwa ndoto pale kiongozi anapokuwa na malengo makubwa huku akiwa na timu isiyostahiki”.Najaribu kumuelewa John C Maxwell,Mchungaji maarufu na miongoni mwa watunzi bora wa vitabu Marekani.Siku zote matokeo bora huletwa na timu bora.Na timu bora ni ile inayofanya kazi kwa pamoja(teamwork).lakini ili upate timu inayocheza kwa pamoja na kwa umoja lazima utengeneze kitu kinachoitwa ‘Chemistry’(kemia)
.
Kwenye soka tumekuwa tukitumia maneno kama chemistry(kemia) huku wengi tukiwa hatujui maana yake.nilishawai kutoa maana ya chemistry wakati naizungumzia Manchester ya van gaal.Nilisema “kemia ni masomo ya atomi na mkusanyo wa atomi kuwa molyekuli.Yaani hizo atomi ukizichanganya utapata kitu kizima kinachoitwa molyekuli. ukichanganya hydrogen na oxygen unapata maji,ukichukua sodium na chlorine unapata chumvi na ukitaka kupata chumvi na maji kwa pamoja ni lazima uchanganye acid na base Mchezaji ndio atomi yenyewe na timu ndio molyekuli.Kitendo cha kuwaunganisha wachezaji katika timu moja na wachezaji hao kuungana katika mfumo husika ndio tunaita chemistry(kemia).Kocha anaposhindwa kupata wachezaji husika kwenye mfumo husika hapo ndipo tunasema kashindwa kutengeneza chemistry kwenye timu.Na kushindwa kupata ‘chemistry’ kwenye timu ndiko kunakofanya timu isicheze kwa maelewano na hapo ndipo tunapokosa teamwork”.
Na hili ndio tatizo kubwa linaloikabili Simba.’Chemistry’ ndio inafanya simba isicheze kwa maelewano.Mechi iliyopita Dhidi ya stand united kikosi cha simba kwenye sehemu ya ulinzi kulikua na wachezaji watano ambao hawajai cheza mechi kwa pamoja,Kiufupi wachezaji wote watano huu ndio msimu wao wa kwanza kucheza simba kwenye ligi kuu,Ukiachana na kipa ‘Cassilas’,Mohamed Hussein,Mugeveke,Isihaka na Miraji ndio ilikua mechi yao ya kwanza kucheza kwa pamoja.Licha ya umri mdogo na kukosa uzoefu kwenye ligi bado mawasiliano yalikua tatizo kubwa kwao,Utaona kabisa atomi hizi zilishindwa kutengeneza molekyuli ya kueleweka.Kama uliwaangalia vizuri kila mtu alikua akicheza anavyojua yeye na si kama timu inavyotakiwa icheze,Tatizo hili lilionekana haswa kwa mabeki wa kati,nawazungumzia Mugeveke na Isihaka.Kama Stand united wangekua na mshambuliaji anayejua kulazimisha mashambulizi kama Danny Mrwanda alivyokua akifanya kwenye mechi dhidi ya Simba basi bila shaka Stand united wangeondoka na ushindi.
Ukiacha Safu ya ulinzi kwenye kiungo pia kuna tatizo hilo hilo la kukosa muunganiko au maelewano kwa lugha nyepesi.Kwizera,Mkude na kisiga ni miongoni wa viungo bora kabisa kwenye ligi kuu Tanzania.Kama ni vipaji hakika Mungu amewapa ,lakini mpaka sasa hawa watu wameshindwa kucheza pamoja kama timu.Kwizera,Kisiga na Mkude ndio mara yao ya kwanza kucheza kwa pamoja kwenye timu moja.Kwa haraka utagundua vipaji hivi maridhawa vimekosa kitu kinachoitwa “Chemistry”.
Nikimuangalia Emmanuel Okwi uwanjani namkumbuka Michael Jordan,Michael Jordan ambaye inasemekana ni mchezaji bora wa kikapu kuwai kutokea ulimwenguni,Jordan kila timu anayoichezea macho yote walikua wakimuangalia yeye.Jordan alikuwa akijitahidi kwa hali na mali timu ishinde lakini mara nyingine timu anayoichezea inapata matokeo mabaya yanayopelekea kukosa kombe.Jordan alikua akiumia sana na siku moja ilibidi avunje ukimya na akasema maneno haya “Kipaji kinaweza kushinda mechi,lakini akili na kufanya kazi kwa pamoja ndipo kunashinda kombe”.Ukiangalia jitihada anazofanya okwi uwanjani ni kama wamemsusia timu.Hapati ushirikiano unaohitajika kutoka kwa wachezaji wenzake,Mpaka sasa Simba imefunga magoli 4 hakuna hata goli moja lisilomuhusisha Okwi.Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua washambuliaji wa simba wamekosa ‘combination’,Hapo ndipo tunarudi kule kule kwenye “Chemistry”