Sakata la vilabu 14 vinavyoshiriki
Ligi Kuu ya Bara kupitia kwa mwanasheria wao, Dk Damas Ndumbaro, kupingana na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya kukatwa asilimia tano ya fedha za
wadhamini wa ligi hiyo na kutishia kutoshiriki ligi na zitapiga kura ya maoni
ya kutokuwa na imani na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ikiwa TFF itatekeleza azma
yake, limechukua sura.
Mapema wiki iliyopita, Malinzi
aliagiza timu hizo kukatwa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo
ya Soka (FDF) ambapo klabu husika zikiwemo Simba na Yanga zimepinga hatua hiyo
na kutishia kutocheza ligi kuu kama agizo hilo litatekelezwa na Bodi ya Ligi.
Sasa kwa mujibu wa vyanzo vya
kuaminika inaelezwa kwamba Shirikisho la soka nchini limefikia hatua ya
kumpeleka mwanasheria huyo Damas Ndumbaro kwenye Kamati ya Nidhamu ya
shirikisho hilo kutokana na kitendo chake alichokifanya mwishoni mwa wiki
iliyopita.