Kocha Patrick Phiri wa klabu ya
Simba SC amesema ni lazima wahakikishe wanapandisha kiwango chao cha uchezaji
haraka kabla ya kuwakabili mahasimu wao wa soka nchini, Yanga SC wiki ijayo.
Simba imelazimishwa sare mara tatu mfululizo na haijapata ushindi wowote msimu
huu. Kiwango cha juu katika mazoezi ambacho kimekuwa kikionyeshwa na wachezaji
wa timu hiyo ni nadra kuonekana katika michezo ya ligi na jambo linalomuumiza
kichwa kocha huyo ni kitendo cha kufunga mabao kisha yanarudishwa.
Simba itacheza na Yanga wiki ijayo na wapinzani wao hao wameshinda michezo miwili iliyopita licha ya kupoteza mchezo wa kwanza siku ya ufunguzi. Nahodha wa timu hiyo Joseph Owino alionekana latika benchi wakati timu hiyo ilipolazimishwa sare na Stand United siku ya JUmamosi iliyopita, ingawa ilifahamika kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda alikuwa na majeraha lakini habari za ndani zinadai kuwa mwalimu huyo aliamua kumuweka nje mlinzi huyo mzoefu baada ya kutoridhishwa na kiwango chake katika michezo miwili ya mwanzo.
“ NImeshazungumza na wachezaji na wanajua kitu gani wanachotakiwa kufanya. Tunahitaji kuboresha kiwango , Simba ni timu kubwa hivyo haipaswi kuzoea matokeo ya namna hiyo”. Alisema, Phiri kocha raia wa Zambia ambaye amewahi kushinda ubingwa wa Bara mara mbili akiwa na timu hiyo miaka ya 2005 na msimu wa 2009/10.
‘” Bila kupandisha kiwango chetu katika siku zilizobaki itakuwa vigumu kuwafunga Yanga ambao wanacheza kwa ushirikiano na wanaonekana kuimarika kadri wanavyocheza. Ni muhimu kwa wachezaji kufanyia kazi mapungufu yaliyoonekana katika michezo mitatu iliyopita. Bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri msimu huu”. Simba imekusanya pointi tatu katika michezo mitatu iliyopita na wapo nyuma ya vinara Mtibwa Sugar kwa tofauti ya pointi sita.