Jose Mourinho alikwepa kumzungumzia mwamuzi, Phil Dowd ambaye alichezesha mchezo wa jana kati ya timu yake ya Chelsea na Manchester United katika uwanja wa Old Trafford. Chelsea iliongoza kwa bao la mshambulizi, Didier Drogba katika dakika ya 53 na ilionekana kama timu hiyo ingeondoka na pointi tatu kabla ya Robbin Van Persie kuisawazishia United katika dakika ya mwisho ya mchezo na kutengeneza sare ya kufungana bao 1-1.
“ Kwa sasa tuna nafasi ndogo kutokana na makosa yetu ama kutokana na makosa ya mwamuzi. Kama nikisema kilicho moyoni mwamgu nitakuwa katika matatizo. Nimechagua kutozungumzia kitendo cha Ivanovic kutolewa kwa kadi nyekundu. Kuna mambo mengi yalikwenda kinyume, na matokeo hayakuwa mazuri kwa upande wetu lakini yanakubalika” alisema, ‘ The Special One’

Chelsea imeendelea kujidhatiti katika msimamo wa ligi kuu ya England, baada ya kucheza michezo tisa ikiwemo dhidi ya timu za Everton, Manchester City na Arsenal, timu hiyo imekusanya pointi 23, pointi nne zaidi ya Southampton walio katika nafasi ya pili, huku wakiwa wamewaacha United kwa pointi kumi. Chelsea haijapoteza mchezo wowote msimu huu na jambo hilo limemfanya., Jose kuwasifu wachezaji wake licha ya kutoshinda Old Trafford.
“ Nina furaha kutokana na timu yangu kucheza vizuri, si rajhisi kucheza dhidi ya United ambao wanacheza mchezo wa kusogeleana huku wakitumia mbinu za kushambulia kwa kushtukiza. Tungeweza kufunga mabao zaidi hasa ile nafasi iliyopotezwa na Hazard. Najivunia wachezaji wangu”.

Drogba alifunga bao katika mchezo wake wa 350 akiiwakilisha Chelsea huku likiwa bao la kwanza msimu huu kwa mchezaji huyo katika ligi kuu. Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast alicheza kwa nguvu muda wote wa dakika 90 ambazo Chelsea ilikosa huduma ya washambuliaji wake, Diego Costa na Loic Remy;
“ Hakuweza kufanya mazoezi na kucheza kwa dakika 90 kama alivyocheza leo ( jana) Nina furaha kumuona akifunga bao, Drogba tayari amefunga mabao mengi kama hili alilofunga”