Klabu
ya Mbeya city Council football Club leo 1/10/2014 imeingia katika
makubaliano na kampuni ya Cocacola Kwanza ya udhamini wa vinywaji
baridi(Official Soft Drink Sponsorship) utakaodumu kwa muda wa miaka 2
wenye thamani ya shilingi 150,000,000.00
Mkataba huo umegawanyika katika maeneo makubwa mawili ambayo ni vinywaji(Maji aina ya Dasani wakati wa mazoezi na mashindano,pamoja na vinywaji vingine kulingana na mahitaji ya klabu vitakavyokuwa na thamani ya shilingi 15m) Pamoja na pesa taslimu shilingi 60m.
Tunaishukuru kampuni ya cocacola Kwanza kwa kuonesha imani hiyo kwetu na kuamua kufanya nasi kazi kwa kipindi hiki cha matazamio.Kampuni ya CocaCola ni kubwa kimataifa na haijawahi kudhamini klabu katika ukanda wetu huu wa Afrika zaidi ya kudhamini mashindano kadhaa,Hivyo tunajiona wenye bahati kuwa moja ya klabu chache kupafanya kazi na kampuni hii kubwa.
Udhamini huu utaimarisha mahusiano ya kampuni na wananchi hasa wapenda michezo,pamoja na kuendelea kujenga imani ya kampuni hii katika tasnia ya michezo nchini.
Kazi kubwa iliyopo mbele yetu kama klabu ni kuendelea kujenga imani hiyo ili fursa nyingi zaidi ziweze kutumiwa na wanamichezo wengine katika michezo mingine hapa nchini.
Nachukua nafasi hii kuwashukuru wote kwa nafasi tofauti waliowezesha mchakato huu wa muda mrefu kukamilika leo,
Nawaomba wapenzi wetu wote popote walipo duniani kuwa mabalozi wazuri kwa kutumia kinywaji baridi cha kampuni ya Cocacola.
“Mbeya City