KIUNGO wa Simba Jonas Mkude anatarajia kurudi dimbani Jumamosi wakati timu yake itakapokuwa ugenini kwenye uwanja wa sokoine ikipambana na Tanzania Prisons katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara.
Daktari wa Simba Yassin Gembe ametoa taarifa kwamba Janas Mkude aliteguka bega lakini kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa vipimo kwenye Hospital ya rufaa ya Muhimbili kitengo cha Moi.
Taarifa za daktari huyo zimempa faraja kocha Patrick Phiri kutokana na mchango mkubwa aliokuwa nao mchezaji huyo katika kikosi cha Simba.
Mkude alitenguka bega wakati Simba ikipambana na Yanga kwenye pambano lililozikutanisha timu zenye upinzani wa jadi Simba na Yanga na kupelekea mchezaji huyo kutolewa nje dakika ya 62 na na fasi yake kuchukuliwa na Pierre Kwizera.