KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amesema timu yake itaingia jijini Mbeya Alhamisi na Ijumaa tayari kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Tanzania Prisons.
Phiri aliyerejea kwa mara ya tatu nchini kuinoa Simba, amesema kikosi chake kinahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kurejesha matumaini yaliyopotea ghafla kutwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuambulia sare
nne mfululizo.
“Tunatarajia kutua Mbeya kati ya Alhamisi na Ijumaa kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ninaamini itakuwa ngumu kwa sababu Prisons iliwahi kuifunga Simba mara mbili na hata Yanga,” amesema kocha huyo.
Msimu uliopita Prisons na Simba zilitoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Februari 9.

Simba inakamata nafasi ya tisa ikiwa na pointi nne baada ya kuambulia sare nne mfululizo katika mechi nne za mwanzo za VPL msimu huu; 2-2 dhidi ya Coastal Union, 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro, 1-1 dhidi ya Stand United na suluhu dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga.
Prisons iko nafasi ya nane ikiwa imeshinda mechi moja dhidi ya Ruvu Shooting, sare dhidi ya Azam FC na vipigo viwili vya 2-1 dhidi ya Yanga na JKT Ruvu. Nafasi ya kwanza inashikiliwa na mabingwa watetezi Azam wenye pointi 10 sawa na mabingwa wa 199 na 200 wa Tanzania Bara, Mtibwa Sugar walioko nafasi ya pili.

Nafasi ya tatu inakamatwa na mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara, Coastal Union wenye pointi saba sawa na Yanga walioko nafasi ya nne wakati Kagera Sugar wako nafasi ya tano wakiwa na pointi tani sawa na Mbeya City na Stand United walioko nafasi za sita na saba.
Mgambo JKT, Polisi Morogoro na Ndanda FC wanakamata nafasi tatu za mwisho baada ya timu hizo kuambulia pointi tatu kila moja kwa kushinda mechi moja katika mechi nne za awali.
Aidha, Phiri amesema kikosi chake bado kinakabiliwa na uwepo wa majeruhi kibao wakiwamo kiungo Jonas Mkude aliyeumia dhidi ya Yanga Jumamosi, mshambuliaji Mkenya Paul Kiongera, beki Nassoro Masou ‘Chollo’ na makipa Ivo Mapunda na Hussein Sharrif ‘Casillas’.