Mwanamuziki wa kimataifa wa Kenya mwenye maskani yake nchini Marekani – Victoria Kimani leo jioni amewasili nchini kwa ajili ya tamasha la Serengeti Fiesta.
Victoria ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake ‘Prokoto’ aliowashirikisha Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz, atakuwa mmoja wa wasanii kadhaa wa kimataifa watakaofanya show kwenye jukwaa la Fiesta jijini Dar Es Salaam siku ya jumamosi katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni.