sitti akiwa amekabidhiwa taji la umiss tanzania kabla ya skendo kujitokeza
Uwezekano mkubwa kuwa hiyo siyo sababu ya ukweli, na mrembo huyo aliona yaishe baada ya kubanwa zaidi na documents na ushahidi mwingine vinavyoonyesha amechakachua umri na akaamua kujiokoa na aibu ya kuvuliwa taji na Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA. Vifuatavyo ni Vielelezo zaidi ya vitatu vinavyoonesha kuwa Sitti Mtemvu alidanganya umri.
Passport yake, leseni ya udereva na taarifa za website rasmi ya ‘Idara ya Usalama wa ndani ya Marekani (Department of Homeland Security), pamoja na profile yake kwenye mtandao wa vipaji, exproletalent.com, vinaonesha kuwa alizaliwa May 31, 1989 na na hivyo kuwa na umri wa miaka 25.