• SIMBAYANGA1
  •  
  • Yanga SC iliyo katika nafasi ya nne itacheza kwa mara ya pili ugenini, katika uwanja ambao timu hiyo ya Dar es Salaam hushangiliwa zaidi ya uwanja wa Taifa, itacheza na wenyeji Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage. Katika mgawanyo wa mashabiki katika Mikoa ya kanda ya Ziwa, Yanga ina idadi kubwa ya wapenzi katika Mkoa wa Shinyanga
  •  
  • Timu iliyozinduka, Coastal Union ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo itakuwa na mchezo mgumu dhidi ya Kagera Sugar. Kikosi cha Yusuph Chippo kimekuwa kitacheza mchezo wa tatu ugenini msimu huu. Baada ya kulazimisha sare na Simba na kulazwa na Mbeya City, Coastal imefanikiwa kukusanya pointi sita katika uwanja wa nyumbani. Kagera chini ya kocha raia wa Uganda, Jackson Mayanja ipo katika nafasi ya tano ikiwa na pointi tano itakuwa ikicheza kwa mara ya pili msimu huu katika uwanja wa nyumbani baada ya kutoa sare ya Stand United wiki iliyopita.
  • azam1
  •  
  • ‘Timu isiyo na kocha’ Ndanda FC itakuwa ikicheza katika uwanja wa nyumbani kwa mara ya pili msimu huu. Ikicheza kwa mara ya kwanza katika ligi kuu msimu huu timu hiyo inashika nafasi ya 12 katika msimamo nafasi ya tatu kutoka mwisho.
  •  
  • Ndanda imeshinda mara moja tu, iliifunga Stand United mabao 4-1 katika uwanja wa Kambarage siku ya ufunguzi lakini haijafanikiwa kushinda tena. Ilifungwa na Mtibwa mabao 3-1 katika uwanja wa Manungu katika wiki ya pili huku wachezaji wake wakihusishwa na imani za kishirikina kiasi cha kusababisha wakatembea kwa kilometa kadhaa kwa miguu wakikatiza katika mashamba ya miwa kwa ‘ hofu ya kulogwa’.
  • blogger-image-1769583005
  •  
  • Mambo yalikuwa nafuu kidogo walipofungwa na Coastal Union kwa mabao 2-1 katika wiki ya tatu katika uwanja wa Mkwakwani, lakini kipigo cha ‘ aibu’ katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona kutoka kwa Ruvu Shooting wiki iliyopita kilisababisha kutimuliwa kati kwa kocha wa timu hiyo, Denis Kitambi na Msaidizi wake, Mwalami Mohammed.
  • Ndanda ilifumgwa mabao 3-1 na Shooting na imekuwa timu ya kwanza kumfuta kazi kocha wake katika ligi kuu msimu huu. Timu hiyo inataraji kumtangaza kocha ‘ Mzawa’ siku ya Jumatatu ijayo itacheza kwa mara yapili katika uwanja wa nyumbani wiki hii dhidi ya JKT Mgambo ya Tanga ‘ timu inayoburuza mkia’ ikiwa imeshinda mara moja kama ilivyo Ndanda.
  • Habari za ndani ambazo nimezipata kutoka katika kambi ya Mgambo ni kwamba uongozi umekuwa ukiwasisitiza wachezaji kushinda mechi. Vichapo vitatu mfululizo vimefanya hata ‘ mambo ya pesa’ kuwa kiduchu kwa wachezaji hivyo wamehakikisha kushinda katika mchezo huo wa pili kwao kucheza ugenini msimu huu.
  • SIMBAYANGA2
  • Ni timu mbili tu miongoni mwa timu zote 14 katika ligi kuu a,bazo hazijapata ushindi hadi sasa, ukitoa Simba ambayo ni miongoni mwa timu tatu ambazo hajizapoteza mchezo wowote ( Azam FC, Mtibwa na Simba hazijapoteza mchezo), Simba haijajishinda katika michezo minne iliyopita, ikiwa inaangaika katika nafasi ya tisa, Polisi Morogoro itakuwa katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi kusaka ushindi wa kwanza msimu huu dhidi ya wenyeji wao, Shooting.
  • Kikosi cha kocha Richard Adolf kikiwa na wachezaji wenye uzoefu kimekuwa na matokeo ‘ butu’. Polisi imecheza mara mbili katika uwanja wa nyumbani, na mara mbili wamecheza ugenini. Timu hiyo iliyo chini ya Jeshi la Polisi haijashinda mchezo wowote, ilifungwa na Azam FC kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kufungua msimu, wakalazimisha sare dhidi ya Simba katika uwanja wa Taifa, mara mbili imetoa sare katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Ilitoa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera kabla ya ‘ kuituliza ‘ Mtibwa kwa suluhu-tasa wiki iliyopita.
  • Watani+22
  • Vinara, Azam FC baada ya kukusanya pointi nne katika michezo miwili waliyocheza katika uwanja wa Sokoine, Mbeya watakuwa katika uwanja wa nyumbani, Azam Complex Chamanzi kucheza na Ruvu JKT iliyo katika nafasi ya 10 ya msimamo. Azam ililazimisha suluhu na Prisons katika wiki ya tatu, kabla ya kuichapa, City kwa bao 1-0 wiki iliyopita. JKT Ruvu ilipata ushindi wa kwanza msimu huu baada ya kuifunga Prisons, siku ya Jumapili iliyopita, kama ilivyo kwa Azam, ushindi wa JKT Ruvu ulipatikana katika uwanja huo huo . Ushindi wa mabao 2-1 ulikuwa wa kwanza kwa kocha Fred Minziro na kikosi chake na mwalimu huyo alisema kuwa wataendelea kushinda.
  •  
  • MSIMAMO WA LIGI KUU BARA ULIVYO BAADA YA MICHEZO MINNE KUPIGWA….
  •  
  • Team;                                   MP,                              W,               D,           L,       PTS
  •  
  • Azam FC                               4                                   3                   1             0         10
  •  
  • Mtibwa                               4                                   3                 1             0         10
  •  
  • Coastal                                4                                   2                   1             1         7
  •  
  • Yanga SC                               4                                   2                   1               1         7
  •  
  • Kagera Sugar                    4                                     1                 2               1         5
  •  
  • Mbeya City                         4                                   1                 2               1           5
  •  
  • Stand United                      4                                   1                 2                 1         5
  •  
  • Tanzania Prisons               4                                     1                 1                 2         4
  •  
  • Simba SC                             4                                    0                   4                 0         4
  •  
  • Jkt Ruvu                               4                                     1                 1                 2         4
  •  
  • Ruvu Shooting                   4                              1                       1                 2           4
  •  
  • Ndanda FC                           4                               1                       0                 3             3
  •  
  • Polisi Morogoro                 4                                0                       3                   1             3
  •  
  • JKT Mgambo                       4                                 1                       0                   3             3
 
Top