Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam FC wameibuka na kusema kuwa mshambulizi wake mahiri na mchezaji bora wa msimu uliopita, Kipre Tchetche hatauzwa wakati huu timu hiyo ikijiimarisha kuelekea michuano ya ndani na ile ya kimataifa. Kulikuwa na habari kuwa Muivory Coast huyo alikuwa mbioni kupigwa bei kwa klabu moja ya Malasyia na nafasi yake kuzibwa na Mmali, Mohammed Traore.
Kupitia msemaji wa timu hiyo, Jaffar Iddi klabu hiyo imesema kuwa Kipre ni mchezaji wao kwa kuwa bado ana mkataba wa miaka miwili zaidi na hakuna ofa rasmi ambayo imefika mezani mwao ili kumuuza mfungaji huyo bora wa msimu wa 2012/13.
Kupitia msemaji wa timu hiyo, Jaffar Iddi klabu hiyo imesema kuwa Kipre ni mchezaji wao kwa kuwa bado ana mkataba wa miaka miwili zaidi na hakuna ofa rasmi ambayo imefika mezani mwao ili kumuuza mfungaji huyo bora wa msimu wa 2012/13.
“ Kipre Tcheche ni mchezaji wa Azam FC, na isitoshe bado ana mkataba na klabu yake ya Azam. Huyu ni mchezaji wetu halali na ataendelea kucheza ligi kuu Tanzan a Bara. Kama kuna timu namuhtaji Kipre taratibu ziko wazi kabisa kuwa klabu inayomuhitaji mchezaji mwenye mkataba inatakiwa kuonana na uongozi wa klabu inayommiliki mchezaji na kukaa kuzungumza. Azam FC yenyewe inaweza kumuuza au isimuuze. Inaweza kumuuza kwa maana kwamba ikiona maslai, au haina maslai.”
“ Kama kuna timu namuhtaji Kipre taratibu ziko wazi kabisa kuwa klabu inayomuhitaji mchezaji mwenye mkataba inatakiwa kuonana na uongozi wa klabu inayommiliki mchezaji na kukaa kuzungumza. Azam FC yenyewe inaweza kumuuza au isimuuze. Inaweza kumuuza kwa maana kwamba ikiona maslai, au haina maslai. Lakini hadi sasa hakuna timu ambayo imewasilisha ofa ya kumuhitaji Kipre kwa maandishi”
Kuhusu usajili wa Traore mshambulizi wa El Merreikh ya Sudan Kaskazini, msemaji huyo wa Azam FC anasema; “ Sisi tunaimarisha kikosi hivi sasa, kwa maana kwamba tunajenga timu ambayo itakuwa na ushindani. Tunakabiliwa na michuano ya klabu bingwa Afrika, na vilevile tunakabiliwa na ligi kuu, tukiwa kama mabingwa watetezi. “
“ Kwa hiyo tunachofanya sasa ni kuhakikisha timu yetu inakuwa na nguvu ili ifanye vizuri. Hatuongezi nguvu kwa maana ya kumuuza Kipre na kumsaini Traore, tunaongeza nguvu kwa maana kuwa akiwepo Kipre pamoja ha Traore tutakuwa na nguvu ya nyongeza katika timu. Tupo kwenye mazungumzo na wachezaji wengi”