Kulekea mchezo wa kesho kati ya Arsenal dhidi ya Manchester United tunakuletea baadhi ya takwimu kuhusiana na mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Emirates.
ARSENAL
The Gunners hawajapoteza mechi hata moja kwenye uwanja wao wa nyumbani msimu huu kwenye ligi kuu ya England, wakiwa wameshinda mara mbili na kutoa sare mara 3 kwenye mechi zao 5 walizocheza Emirates Stadium.

Rekodi ya Manchester United kwenye viwanja vya ugenini ni mbovu mno. wameshindwa kushinda katika mechi zao tano kwenye ligi wanapocheza ugenini msimu huu.
Alexis Sanchez yupo on fire, amefunga magoli sita katika mechi 4 zilizopita za ligi kuu.
MAN UNITED
United hawajapoteza mechi hata moja katika 3 za mwisho walizotembelea uwanja wa Emirates Stadium.
United hawajapoteza mechi hata moja katika 3 za mwisho walizotembelea uwanja wa Emirates Stadium.
Arsenal hawajaifunga United katika mechi zao sita zilizopita.
United hawajapoteza mechi hata moja katika mechi 18 zilizopita dhidi ya vijana wa Arsenal Wenger.
MATOKEO YA MECHI 4 ZILIZOPITA
February 12 2014: Arsenal 0-0 Manchester United
November 10 2013: Manchester United 1-0 Arsenal – van Persie (27)
April 28 2013: Arsenal 1-1 Manchester United – Walcott (2); van Persie (44)
November 3 2012: Manchester United 2-1 Arsenal – van Persie (3), Evra (67); Cazorla (90+5)