BAADA ya kupata pigo kwa wachezaji wake saba kukacha soka kwa muda na
kutimkia kwenye mafunzo ya kijeshi, Kikosi cha Ruvu Shooting
kimefanikiwa kumnasa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram Mwombeki na
muda wowote kitamsainisha mkataba wa mwaka mmoja.
Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire amesema jijini Dar es Salaam leo mchana kuwa uongozi wa timu hiyo umeamua kumsajili mshambuliaji huyo aliyekuwa huru baada ya kuachwa na Simba msimu uliopita ili kuziba pengo lililoachwa na wachezaji wao saba ambao wamepelekwa kambi ya mafunzo maalum ya kijeshi.
Ruvu Shooting inamilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Kitengo cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Bwire amesema wengi wa wachezaji wao walioondoka ni washambuliaji hivyo bado wanasaka mshambuliaji mwingine kama ilivyopendekezwa ma kocha wao Mkenya Tom Olaba.
“Ni jambo la kawaida kwetu ukizingatia hii ni timu ya jeshi, wachezaji wanakwenda kwenye shughuli nyingine za nje ya soka. Katika wachezaji 30 tuliowasajili msimu huu, wameondoka hao saba, tutaziba pengo. Kikubwa hatufanyi usajili wa kibabaishaji, kikosi chetu bado kiko imara,” amesema Bwire.
“Siwezi kuwataja kwa majina kwa sababu mimi si msemaji wa jeshi, lakini wengi wao washambuliaji ndiyo maana leo tumeamua kumpa mkataba wa mwaka mmoja Mwombeki maana kocha ameagiza tusajili washambuliaji wawili dirisha dogo ili wasaidiane na washambuliaji wachache waliobaki.
“Mwombeki ilikuwa leo asaini lakini wakala wake amemzuia na amemtaka waonane kwanza kabla ya kuusaini mkataba wetu. Amesema kesho atasafiri kwenda Mwanza kuonana na wakala wake na baada ya siku tatu atarejea na kuusaini,” amesema zaidi Bwire.
Mwombeki alipata wakati mgumu akiwa Simba chini ya kocha aliyetimuliwa Agosti 10, mwaka huu, Mcroatia Zdravko Logarusic ambaye ilifikia kipindi akamuingiza kisha kumtoa baada ya dakika tatu.
Msimu uliopita, baadhi ya wachezaji wa Ruvu Shooting walitimkia Uarabuni kusaka nafasi ya kucheza soka la kulipwa ughaibuni, jambo ambalo hawakufanikiwa, hata hivyo.