Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Timu ya Taifa ya Morocco imeondolewa katika michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2015, kutokana na maamuzi ya nchi hiyo kujitoa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo yaliyotarajiwa kuanza Januari mwakani, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limethibitisha leo baada ya kukutana jijini Cairo, Misri jana.
Nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika ilifikia maamuzi ya kujitoa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Bara la Afrika kwa kuonesha hofu ya kuenea kwa Ebola, ugonjwa ambao umelipuka Magharibi mwa Afrika.
CAF imesisitiza kuwa michuano hiyo itaendelea bila kubadilishwa ratiba na kwamba nchi mwenyeji/ wenyeji zitawekwa wazi muda wowote.
TAARIFA YA CAF INASOMEKA:
Katika mkutano wa Novemba 11, 2014 jijini Cairo, Kamati ya Utendaji ya CAF iliamua kuchukua maamuzi kuhusu tamko la Waziri wa Vijana na Michezo wa Morocco kufuatia katika barua yake ya Novemba 8, 2014 waliyoomba kuahirishwa kwa Afcon 2015.
Maombi hayo yalithibitisha kwamba Shirikisho la Soka la Morocco haliko tayari kuandaa mashindano katika tarehe iliyopangwa (Januari 17-Februari 8, 2015).
Kwa hiyo, kwa kuwa wamejibu baada ya kuwakumbusha pia Novemba 3 kuandaa michuano katika tarehe iliyopangwa, Kamati ya Utendaji imeamua michuano ya Afcon 2015 haitafanyika Morocco.
Kamati ya Maandalizi ya Afcon baadaye itatoa mwongozo kwa kile kinachopaswa kuchukuliwa baada ya Shirikisho la Soka la Morocco kuvunja makubaliano na kwenda kinyume cha makubaliano, ikiwa ni pamoja na makubaliano ambayo shirikisho, Serikali ya Misri na shirikisho hilo walisainiana na CAF April 2014.
Kamati ya Utendaji ilitangaza 10 Novemba, 2014 kuanza kupokea maombi ya nchi wanachama wa CAF kuandaa Afcon 2015 kwa masharti kuwa watakuwa tayari kuwa wenyeji wa mashindano hayo katika tarehe zilizopangwa. Kamati itafanya maamuzi baadaye baada ya kupokea maom,bi hayo.
Kamati ya Utendaji inathibitisha kuwa mechi za kuwania kufuzu mwezi huu (Novemba 14/15 na Novemba 19), zitaendelea kupata timu 15 zitakazoungana na nchi mwenyeji.
Mathalani, kufuatia kujitoa kwa Nchi ya Morocco kuwa mwenyeji, Kamati ya Utendaji imeamua kuwa Timu ya Taifa ya Morocco moja kwa moja imeondolewa na haitashiriki michuano ya 30 ya Afcon mwakani